HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 1, 2011

Uzinduzi wa nyumba poa kigamboni

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Nyumba Poa Huko Kigamboni Jijini Dar es salaam jana, Mradi huo unaendeshwa na Kampuni ya Nyumba Poa LTD inayoendeshwa na vijana Watanzaia walioamua kutoka Ughaibuni na kurudi nyumbani ili kuwekeza katika kusaidia kukuza uchumi wa nchi yao lakini pia kusaidia jamii katika kupata nyumba bora kwa bei nafuu.

Nyumba iliyozinduliwa inagharimu Milioni 25 za Tanzania na inaweza kupanda kutegemea na mahitaji ya mteja mwenyewe anataka nini kiongezeke katika kuboresha zaidi nyumba yake, Lakini pia nyumba hizo zimebuniwa ili kusaidia watu wenye kupato cha kawaida ambao kwa upande wao kujenga inakuwa ni kazi ngumu hivyo kupitia mradi huu wa Nyumba Poa Model House watu wa kipato cha chini wanaweza kujipatia nyumba bila matatizo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mh. Bernald Membe ameishukuru kampuni ya Nyumba Poa LTD kwa kuanzisha mradi huo hapa nyumbani kwani wameamua kuitikia wito wa serikali na kuja kuwekeza nyumbani, amesema Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete pamoja na yeye mwenye wamekuwa wakiwaasa Watanzania wengi walioko nje ya nchi kurudi nyumbani na kuwekeza au kuwekeza nyumbani wakiwa hukohuko nje jambo ambalo Kampuni ya Nyumba Poa LTD imeitikia kwa vitendo.

Wanaoshuhudia ukataji wa utepe kutoka kulia ni Daniel Mziray Mkurugenzi wa ufundi wa Kampuni ya Nyumba Poa LTD na Peter Malika Mkurugenzi wa Kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Nyumba Poa LTD Bw. Peter Malika akizungumza katika uzinduzi huo na kutambulisha wafanyakazi wenzake wa kampu ni hiyo hawapo pichani ambapo alisema kuna wataalamu wa nyanja tofauti.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Nyumba Poa LTD Bw. Daniel Mziray akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kiamataifa wakati alipokuwa akitembelea na kujionea nyumba hiyo.
Nyumba ya mfano na iko katika hatua za mwisho za umaliziaji ili kukamilikakabisa ni nyumba nzuri na ya bei rahisi lakini ina vyumba vitatu bafu na choo ndani huku mkukiwa na jiko pamoja na sebure.
Waziri Bernald Membe akiwasikiliza Investors Strateges Partiner wa Kampuni ya Nyumba Poa kushoto anayezungumza ni Gerald Heyder na katikati ni Pramod KumarJain wa Interglobe Export Corp.ya New York Marekani.
Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika uzindzu huo wakifuatilia kwa makini kila kilichoendelea katika uzindzu huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad