HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 31, 2011

MATOKEO : MAONI YA WATU KUHUSU TIBA YA BABU LOLIONDO


Habari Bro Othman
Tunashukuru sana kwa kuwekea tafiti yetu kwenye blog yako. Leo ndio ile siku ya kutangaza matokeo. Chini ni ujumbe unaoambatana na link ya kwenye maoni. Pia tumeattach picha ambayo unaweza kuambatanoisha na hii post. Tunatanguliza shukrani mkuu.
...............................................................................................

MATOKEO : MAONI YA WATU KUHUSU TIBA YA BABU LOLIONDO
Kwa niaba ya Bongo Promotions tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wale wote walioshiriki katika survey tuliyoitangaza siku ya jumatatu (28.03.11). Lengo la kufanya huu utafiti mdogo ni kuangalia mitizamo ya wananchi kuhusu tiba ya babu Loliondo.

Tumepata maoni mengi sana kutoka kwa watu zaidi ya 180. Takwimu zinaonyesha wengi wamependekeza kwamba taratibu za kitaalam zifanyike kuthibitisha kama dawa inatibu, wengine wanasema kuwa hili ni suala la imani zaidi. Wapo walio fedheheshwa na juhudi za vingozi kutokuwa za kuridhisha katika kufuatilia suala hili na badala yake wao kuwa ni miongoni wa wanaojitokeza kwenda kupata kikombe. Unaweza kupata maelezo zaidi na report kamili ya hii tafiti ndogo kupitia link hiyo hapo chini.


Tunashukuru kwa ushirikiano wako
BONGO PROMOTIONS Team

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad