HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 28, 2011

WAZIRI MKUU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MABOMU GONGO LA MBOTO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akizungumza na wakazi wa Gongolamboto (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuwaona waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya JWTZ Gongolamboto leo jijini Dar es salaam ambapo ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika na ugawaji wa misaada kuhakikisha kuwa misaada hiyo inawafikia walengwa.
Wajasilia mali wa kikundi cha SEUMA kutoka Segerea jijini Dar es salaam wakimkabidhi Waziri mkuu Mizengo Pinda msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa milipuko ya mabomu ya Gongolamboto leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa nne kulia) Pinda akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Gabriel Fuime(wa sita kushoto) kuhusu upokeaji na uhifadhi wa misaada mbalimbali inayotolewa kuwasaidia waathirika wa mabomu Gongolamboto inavyohifadhiwa na kugawiwa kwa walengwa husika leo eneo la Shule ya Sekondari Pugu jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi akikabidhi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa tani 17 za vyakula mbalimbali na hundi ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea eneo la Gongolamboto.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya wananchi wa Majohe ambao nyumba zao ziliharibiwa na mabomu yaliyolipuka katika kambi ya JWTZ ya Gongolamboto hivi karibuni wakati alipoeatembelea leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia moja ya nyumba iliyoteketea kwa moto kutokana na milipuko ya mabomu eneo la Majohe leo jijini Dar es salaam.
Wasanii wa Muziki na Filamu wakipita mbele ya Waziri mkuu Mizengo Pinda na kuwasilisha michango mbalimbali ya fedha na vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 76 waliyoipata kutokana na tamasha walilolifanya kuchangia waathirika wa Mabomu katika eneo la Gongolamboto jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)akizungumza na baadhi ya familia za waathirika wa milipuko ya mabomu eneo la Majohe leo jijini Dar es salaam na kuwahakikishia kuwa serikali itafanya kila linalowezekana kuwasaidia.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad