HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 28, 2011

Kampuni ya bahati nasibu ya Premier Betting yatoa msaada kwa wahanga wa gongo la mboto

Kampuni ya bahati nasibu ya Premier Betting kupitia mchezo wake wa Premier Bingo imekabidhi msaada kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto msaada huo ni wa thamani ya shilingi milioni moja.

Akikabidhi msaada huo kwa mratibu wa misaada wa kituo cha Clouds FM Muhidin Mrope Meneja Masoko wa kampuni hiyo Afsa Hamad alisema kuwa kampuni ya Premier Betting imeguswa na matatizo yanayowagusa waathirika wa Gongo la Mboto.

Msaada huo ni mipira 22, kilo mia mia za mchele, sukari, maharage na gunia mbili za sabuni ya unga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad