
Mwenyekiti wa Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF),Bw. Hassan Mitawi akikabidhi tuzo kwa Meneja wa Steps Entertainment,Ignatus Kambarageya aliemuwakilisha Mtoto Hanifa Daud alieibuka muigizaji bora katika filamu ya THIS IS IT.

Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF),Prof. Martin Mhando akiongea wakati wa utoaji tuzo kwa filamu mbili bora kati ya nane zilizokuwa zikishindanishwa katika tamasha dogo la ZIFF (ZIFF Mini- Festival).filamu zilizofanyikiwa kupata tuzo ni HUBA iliyotengenezwa na PiliPili Entertainment na THIS IS IT ya Steven Kanumba kutoka Steps Entertainment.tamasha hili limemalizika usiku wa kuamkia leo katka viwanja vya ngome kongwe,Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF),Bw. Hassan Mitawi akiongea wakati wa utoaji tuzo kwa filamu mbili bora katika tamasha dogo la ZIFF (ZIFF Mini- Festival) lililomalizika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya ngome kongwe,Zanzibar.

Mkurugenzi wa PiliPili Entertainment,Sameer Srivastava (kushoto) pamoja na Meneja Steps Entertainment,Ignatus Kambarage wakionyesha tuzo za filamu walizozitengeneza usiku wa kuamkia leo.filamu hizo pia zimepata nafasi ya kushiriki Tamasha la Filamu la Afrika litakalofanyika nchini Burkinafaso mwezi Februari.katikati ni Mke wa Mkurugeni wa PiliPili Entartainment.


Kijana Fareed Abdullah wa kundi la B6 la visiwani Zanzibar,akionyesha umahiri wake wa kuyarudi majoka kama aliyokuwa akiyarudi Marehemu Michael Jackson enzi za uhai wake.kijana huyu anazidi kujinyakulia umaarufu visiwani hapa kwa uwezo wake huo wa kumuigiza Michael Jackson.

Vijana wa kundi la B6 wakionyesha mambo yao.

No comments:
Post a Comment