
Nipo Visiwani Zanzibar kwa muendelezo wa libeneke la Mtaa Kwa Mtaa na hapa mtalii wa ndani mie nikiwa katika moja ya vifaa vilivyotumika katika vita miaka ya zamani,vilivyopo katika jengo la Maajabu,Mji Mkongwe..

Ankal Lukwangule nae huwa nyuma katika kukati kiu kwa juisi ya miwa.

Forodhani ndio sehemu pekee ya kurekebisha swala zima la tumbo nyakati za usiku katika mji huu wa Zanzibar,hapa nikipata kitu cha juisi ya miwa na miskaki ya kukuzz.

Mchana wa leo katika libeneke la mtaa kwa mtaa ndani ya mji mkongwe.

Wadau wa kijiji cha Jirani cha FotoBaraza,toka shoto ni Babukadja,Grey,Ekonjo,Mie pamoja na mdau Ahmad tukipata lanchi ya pamoja katika kiota cha CCM mchana wa leo.

chombo kikiwa kimetia nanga bandarini.


Mitaa ya Mji Mkongwe mchana wa leo.

Jengo la Hospital ya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar leo.

Maalim akiwahi chombo.

Boda Boda ya kihome home ikiwahi mahala.

Usafiri wa Punda hutumika sana katika visiwa hivi vya Zanzibar kama kamera ya mtaa kwa mtaa ilivyokutana na taswira hii.

Msela akiwaimbisha watasha ili waweze kununua moja ya vinyago alivyokuwa akiviuza.




Unavyoonekana Mji Mkongwe.
No comments:
Post a Comment