Mhe. William Lukuvi,Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) (pichani) atatembelea ofisi ya Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya kesho tarehe 07/01/2011 siku ya Ijumaa saa 3 Asubuhi.
Mhe, Lukuvi atatembelea Ofisi hizo za Tume zilizopo Upanga, barabara ya Mariki kitalu Na. 434, kupata taarifa ya utendaji wa kazi na kutoa maelekezo ya utendaji huo wa shughuli za kila siku za Tume katika kutekeleza jukumu lake la Kuratibu udhibiti wa dawa za kulevya ikiwa ni moja ya taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment