HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 5, 2011

wakutanapo wawili hawa,huwa hashindwi mtu

Jamaa mmoja, Nshomile aliwakuta rafiki zake wawili wahaya wakiwa katika mazungumzo ya kawaida.

Mmoja wao alikuwa ana mtoto anaitwa Gosbert ambaye alisoma shule ya msingi na huyu Nshomile.

Mazungumzo yakawa hivi:-

Nshomile: Ndugu yangu za siku, Mwanao hajambo?

Baba Gosbert: Salama, Mwanao pia vipi?

Nshomile: ..Aaah Livingstone anaendelea vizuri, baada ya primary kalifaulu kwenda Mzumbe, kule kakaperform vizuri sana. High school alikwenda Ilboru akatoka na pointi tatu. wakamchagua Muhimbili, he did wonders akagraduate as a best student, akasomea shahada ya uzamili makerere, sasa ni surgeon, daktari bingwa wa upasuaji. Vipi ka Gosbert, kako wapi siku hizi?

Baba Gosbert: (kwa kujiamini) Aah Gosbert pia alifanya vizuri sana, kwa sasa anashughulikia wagonjwa walioshindikana na mabingwa!

Nshomile:haya kwaherini, (akaaga akiwa mnyonge, aliamini kuwa mwanae Livingstone ana mafanikio zaidi ya Gosbert)

Baada ya kuondoka, yule jamaa watatu akamuuliza Baba Gosbert; Hivi kumbe ka Gosbert kamesoma eeh!

Baba Gosbert:...ah, kapumbavu sana kasome wapi? Kameishia kuchimba makaburi tu!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad