
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu - Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi akiongea na waandishi wa habari na baadhi ya maafisa wa Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za Kulevya Nchini pindi alipotembelea tume hiyo leo jijini Dar es salaam. Waziri Lukuvi amesema kuwa tume hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kuthibiti uingiaji wa biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na udhaifu wa sheria iliyopo ya kupambana na kuthibiti dawa za kulevya ambapo amesema kuwa serikali itaunda timu itakayotoa mapendekezo kuhusu uimarishaji wa sera, muundo na urekebishaji wa sheria ya kudhibiti dawa za kulevya ya mwaka 1995 ili kutoa uwezo kwa Tume hiyo kuwashughulikia mara moja watakaojihusisha na biashara hiyo.

Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher J. Shekiondo akitoa Taarifa ya utendaji kazi wa Tume ya Kuratibu na kudhibiti Dawa za kulevya kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu -Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi (kushoto) leo jijini Dare salaam ambapo ametoa wito kwa wananchi kuwafichua wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Baadhi ya wanahabari na maofisa wa Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za kulevya wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu -Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi leo jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment