
La Mizoga likiwa limenyanyuka tairi za mbele wakati likijaribu kuchomoa gari ya Tanesco iliyochomekewa na kuingia mtaroni maeneo ya Manyanya,Kinondoni jijini Dar.

Kitu ndio kimetulia hiyoo,ila cha kushukuru Mungu ni kwamba hakuna alieumia wala kupoteza maisha katika ajali hii.

Askari wa usalama Barabarani akichukua maelezo toka kwa dereva wa gari hiyo.

Utaratibu wa Kuitoa gari hii mtaroni ukiendelea .

Mashuhuda kama kawa,huwaga haachezi mbali na matukio kama haya.
Tatizo la sisi wabongo hata siku moja hatuulizi kwa nini serikali ya jiji haifuniki hiyo mitaro!! Hiyo mitaro ni hatari kwa magari pamoja na watembea kwa miguu, watoto wadogo kutumbukia humo, nk. Miaka yote tunaiona na kuichekea tu. Bongo tubadilike, tudai serikali za majiji au serikali kuu kufunika hiyo mitaro. Ni pesa zetu walipa kodi.
ReplyDelete