HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 16, 2010

safari ya mwisho ya dr. remmy mtoro ongala

Marehemu Dr. Remmy Ongala enzi za uhai wake.
Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo, Dr. Emmanuel Nchimbi akisema machache wakati wa kuaga mwili wa marehemu Dr. Remmy Ongala katika viwanja vya Biafra,Kinondoni Jijini Dar.
Jeneza lililohifadhiwa mwili wa Marehemu Dr. Remmy Ongala likiwa limewekwa sehemu maalum kwa ajili ya kuagwa.
Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Dr. Remmy Ongala leo kwenye ibada iliyofanyika katika viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar.
Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Ubungo na Kinondoni.Mh. John Mnyika pamoja na Mh. Iddy Azan wakipita kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Dr. Remmy Ongala leo.
Wanafamilia wakitoa heshima zao za mwisho.
Mmoja wa watoto wa Marehemu Dr. Remmy Ongala,Kaliomangonga Ongala akifungua Jeneza lenye Mwili wa Baba yake tayari kwa taratibu za kutoa heshima za mwisho.
Mwanamuziki Mkongwe na aliekuwa pamoja na Marehemu Dr. Remmy Ongala,Bw. Cosmas Chidumule akiongea na Waziri wa Habari ,Utamaduni na Michezo,Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi juu ya udhibiti wa haki za wasanii wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Dr. Remmy Ongala katika viwanja vya biafra,Kinondoni jijini Dar leo.
Askofu wa Kanisa la Pentekosti,David Mwasota akitoa neo la mungu katika ibada ya kumuaga mkongwe wa Muziki wa Dansi hapa nchini,Marehemu Dr. Remmy Ongala,iliyofanyika katika viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar leo.
Mke wa Marehemu Dr. Remmy Ongala akiwa ni Mwenye majonzi makubwa kwa kumpoteza mumewe.
Mzee Kitime na Mzee Makassi wakijadiliana maswala mawili matatu katika shughuli hiyo.
Jukwaa wa Waheshimiwa na wageni mbali mbali.
Mkongwe katika Libeneke la Dansi Nchini,Cosmas Chidumule alizungumzia maswala mbali mbali aliyokuwa akiyafanya pamoja na Marehemu Dr. Remmy Ongala.
Ankal akiwa na wakongwe katika libeneke la Muziki wa Dansi hapa nchini.
Familia ya Marehemu Dr. Remmy Ongala ikiwa katika majonzi makubwa kwa kumpoteza kipenzi chao na kipenzi cha watu wengi,Dr. Remmy Ongala ambaye atakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya enzi za uhai wake.
Wanausalama pia walikuwepo kuhakikisha usalama unapatikaka katika eneo hilo.
Ankal akihaha huku na kule kuhakikisha kideo kinapatikana cha uhakika.
Wadau mbali mbali walikuwepo katika kuaga mwili wa Dr. Remmy Ongala leo.
Huzuni ilitawala kwa kila mtu aliefika katika viwanja vya Biafra kuuaga mwili wa Marehemu Dr. Remmy Ongala leo.
Umati mkubwaa ulijitokeza katika viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar leo ili kuuaga mwili wa Marehemu Dr. Remmy Ongala.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad