
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Dietlof Mare akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania kwa kutoa huduma ya miaka kumi nchini Tanzania.hafla hii imefanyika asubuhi ya leo katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akitoa ufafanuzi katika mkutano na waandishi wa habari juu ya mtandao wa Vodacom utakavyoboreshwa baada ya kutoa huduma zake kwa muda wa miaka kumi hapa nchini.

Mkurugenzi wa uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akikaribisha maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari waliofikam leo katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski wakati wa mkutano wa Vodacom kusherehekea miaka kumi kwa kutoa huduma zake hapa nchini.

Baadhi ya wakurugenzi wa Vodacom Tanzania wakijibu maswali mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Dietlof Mare wa tatu kutoka kushoto.

Baadhi ya wakurugenzi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika sherehe ya Vodacom kutimiza miaka kumi ya kutoa huduma zake hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Dietlof Mare akijibu moja ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari waliofika leo katika ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro Kempiski kwenye sherehe ya kumitimiza miaka kumi ya huduma za Vodacom hapa nchini.Kulia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Vodacom,Exaudi Kiwali na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephrahim Mafuru.

Wadau wa Vodacom wakibadilisana mawazao mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutimiza miaka kumi ya huduma za Vodacom nchini.

Stori za hapa na pale zilitawala katika hafla ya kutimiza miaka kumi ya huduma za Vodacom hapa nchini.
No comments:
Post a Comment