Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,Dr Patrick Makungu akizindua huduma mpya ya Tigo Pre Paid Blackberry leo kwenye hafla fupi iliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.Dr Patrick ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi alisema kuwa "Ninayo furaha kubwa kuwa nanyi mchana huu wa leo ambapo Tigo mnazindua huduma kabambe ya malipo ya kabla ya mtandao wa intanet ya backberry kupitia mtandao wa Tigo – Tigo Pre paid blackberry.
Kwa niaba ya serikali kupitia wizara ya mawasiliano sayansi na teknolojia kwanza niwapongeze kwa hatua hii nzuri mliofikia ya kuamua kuleta huduma hii ya blackberry malipo ya kabla ambayo kama mlivyosema mmeitikia ombi toka kwa wateja mnaowahudumia Pili ninawapongeza kwa kuweka vifurushi vya viwango vya chini zaidi na nafuu kuliko mtandao wowote nchini katika huduma hii ya backberry malipo ya kabla .
Kubwa zaidi ni kwamba ninyi mmeweka kiwango cha chini kabisa cha kulipia shilingi elfu saba tu kwa siku saba na mteja akafurahia huduma ya intaneti! Hongereni kwa hilo, Hayo yote ni mafanikio na ndio maana hata mlitunukiwa ubora wa huduma za mawasiliano nchini na wataalamu wanaofanya utafiti kwenye zaidi ya nchi 80 “Superbrand” hivyo yote hayo ni matunda ya uwekezaji wenu kwa wateja wenu kutokana na bidhaa mnazowapatia .
Hivyo sasa kwa niaba ya serikali ninawaomba muendelee kusaidia jamii kwa kuboresha mawasiliano yawe ya kisasa zaidi kwa kuibuka na vitu vipya vingi vitakavyorahisisha mawasiliano na kupitia hilo wananchi waweze kuboresha maisha yao ya kila siku kwa kuwa shughuli zetu za kila siku zinategemea sana mawasiliano Baada ya kusema haya machache naomba nitamke rasmi kuwa huduma hii ya Tigo Blackbery ya malipo ya kabla imezinduliwa rasmi .

Afisa viwango wa huduma za Tigo,Bw. David Zakaria akifafanua jambo kwa undani zaidi namna ya kujiunga na kutumia huduma ya Blackberry kutoka Tigo,mbele ya wageni waalikwa na waandishi wa habari katika hafla fupi iliofanyika kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Kempinsk,jijini Dar.

Mkurugenzi wa masoko wa Tigo Bw. Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kuhusiana na huduma yao mpya ya Blackberry walioizindua leo,uzinduzi huo ulifanyika kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Kempinsk,jijini Dar.

Pichani kusho ni Afisa mahusiano wa Tigo,Jakson Mmbando akimuelekeza jambo Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,Dr Patrick Makungu kabla ya kumpa mwanalibeneke mwenzetu alijishindia Blackberry hiyo leo ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya Kempisk,jijini Dar
We absolutely love your blog and find almost all of your post’s to be just what I’m looking for.
ReplyDeleteDoes one offer guest writers to write content for you personally?
I wouldn’t mind publishing a post or elaborating on a number of the subjects you write with regards to here.
Again, awesome web log!
섯다