HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 28, 2010

“Origin Africa” kuonesha mavazi wakati wa Swahili Fashion Week


Onesho la mavazi kutoka The “Origin Africa” kupitia la Swahili Fashion Week litafanyika tarehe 5 ya mwezi November 2010, Dar es Salaam katika Bustani ya Karimjee Gardens , ikiwa ni siku ya pili ya jukwaa la kubwa la maonesho ya mavazi Tanzania linalojukikana kwa jina la Swahili Fashion Week.

“Origin Africa” ni project iliyo chini ya USAID East Africa Competitiveness and Trade Expansion Program (COMPETE) Dhana nzima ya Origin Africa ni kuichukua staili ya kiafrika na kuipekeka katika hali ya usasa.

Origin Africa inalenga katika kutoa uelewa kwamba Afrika ni chanzo kizuri cha biashara na kudadilisha dhana ya biashara kwa kulenga wanunuzi wa kimataifa, viongozi wa kibiashara na wabunifu kwa ujumla.

Pia kutoa nafasi kwa wabunifu mbalimbali kuonesha vipaji yao jukwaani, kubadilishana nawazo na uzoufu pamoja na kujitngaza kwa upana zaidi kwa kuonesha ubunifu wa hali ya juu.

“Onesho la The “Origin Africa” litawaleta pamoja wabunifu kutoka kanda ya Africa Mashariki kuonesha ubunifu wao wa asili katika jukwa la kimataifa. Tunaamini kwamba tutaleta hamasa na kuibua nafasi mbalimbali kwa vipaji vipya katika fani ya mitindo, kwa wabunifu kufanya kazi pamoja na kukuza Sanaa ya mitido katika bara la Africa.” Alisema Mustafa Hassanali, muandaaji wa Swahili fashion week.

“USAID/COMPETE kupitia East and Central Africa Trade Hub inasaidia masuala ya ufundi kwa taasisi za kibiashara Africa na Serikali katika kuhamasisha kuwepo kwa ushindani wa masoko kidunia, sambamba na kuchangia kupatikana kwa nafasi mbalimbali za kibiashara na kusaidia wafanyabiashara wa Africa kupata nafasi mbalimbali za masoko, chini ya mpango wa AGOA (African Growth and Opportunity Act).

The ECA Hub imejenga uhusiano wa karibu wa kikanda na waashirika mbalimbali katika kupanua uigo wa uuzaji wa bidhaa na muningiliano kibiashara.” Alisema Ndugu Finn Holm-Olsen, Mkurugenzi wa Tthe East and Central Africa Trade Hub.

“Siku ya mwisho ya Swahili Fashion Week, USAID/COMPETE itaandaa workshop itakayotoa taaluma kwa wabunifu katika suala zima la muonekano bora katika fashion shoo kwa vitu vinavyotengeneza na wabunifu, pia mafunzo yatakayosaidi katika kutoa miongozo ya kueleke katika mauzo, na kuangali suala zima la masoko kwa ujumla.

Workshop hiyo pia itaangalia kwa jinsi gani wabunifu wanaweza kupata nafasi katika masoko nchini Marekani na ya kimataifa kwa ujumla, sambamba na kukuza ubunifu hapa nchini na hata kuvuka mipaka hadi nje ya nchi.” Alisema Mr Holm-Olsen.

Workshop hiyo itafanyika katika hotel ya Southern Sun Hotel, tarehe 6 November na itawashirikisa wabunifu wote ambao wameshiriki katika Swahili Fashion Week, kwa wale wanaochipukia na hata kwa wale ambao na wakongwe katika fani ya ubunifu.

“ Kama wabunifu wengi wataonesha mavazi, kitaifa na kimataifa, waliyoyabuni kwa kutumia malighafi zinazozalishwa na viwanda vya nguo vilivyopo katika kanda hii, hali itakayoleta faida kwa viwanda vya nguo vilivyopo Africa Mashariki.

Na huu utakuwa mwanzo mzuri na endelevu katika sekta hii.” Alisema Bwana Barry Fisher, USAID/COMPETE’s Senior Cotton/Textile/Apparel Specialist.

“ Tunategemea kwamba siku moja sekta hii ya Fashion kwa Afrika Mshariki itakuwa zaidi na kutambulika kuwa kiungo bora kwa sekta ya viwanda na kuwa moja ya wachangiaji wakubwa wa uchumi kwa kanda hii.” alisema Mustafa Hassanali, muandaaji wa jukwaa la Swahili Fashion Week.

“Origin Africa na Swahili Fashion Week inatoa fursa kwa wabunifu wa kuonesha ubunifu wao, na kuwapa taaluma katika masuala ya mauzo kwa ujumla. Hii ni nafasi adhimu kwa wabunifu kuitumia ipasavyo katika kuonesha vipaji vyao, na pia kupata fursa ya kubadilishana ozoefu na kuitangaza kimataifa kwa upana zaidi African Fashion.” Aliongeza Bwana Fisher.

Kuhusu Swahili Fashion Week

Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

Swahili fashion week in tukio ambalo linawajumuisha wabunifu wakongwe na wale wanaochipukia kuonyesha kazi zao, pia kutoa nafasi kwa wapenzi wote wa sanaa ya mavazi kujumuika pamoja na kufurahia ubunifu wa watanzania na kutoka nchi za jirani.

“Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kuwa sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa na kwa nchi za Afrika Mahariki”. Alifafanua Mustafa Muanzilishi na Muuandaaji wa Swahili Fashion Week.

Kuhusu “Origin Africa”

“Origin Africa” ni project iliyochini ya USAID East Africa Competitiveness and Trade Expansion Program (COMPETE). Dhana nzima ya Origin Africa ni kuichukua staili ya kiafrika na kuipekeka katika hali ya usasa.

Origin Africa inalenga katika kutoa uelewa wa kwamba Afrika ni chanzo kizuri cha biashara na kudadilisha dhana ya biashara ya kwa kulenga wanunuzi wa kimataifa viongozi wa kibiashara na wabunifu kwa ujumla.

Kuhusu USAID /COMPETE

USAID /COMPETE, ipo Nairobi, Kenya, na imekuwa ikifanya kazi Afrika Mahariki na kata, kwa lengo la kupunguza vikwazo vilivyopo katika biashara na kusadia kampuni mbalimbali za kiafrika kuingia katika ushindani kibiashara kikanda na kimataifa.

USAID/COMPETE’s East and Central Africa Trade Hub inawasaidia wafanyabiashara wa Afrika kupata nafasi mbalimbali zilizopo chini ya mpango wa African Growth and Opportunity Act (AGOA).

Kwa miezi 18 sasa, ECA Hub imeshatumia dolla zisizopungua $25 millioni of exports in apparel, kukata maua, masuala ya utengenezaji chakula, sanaa ya uchongaji na mampambo chini ya mpango wa AGOA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad