HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 28, 2010

hoja ya mdau

Habari wakuu!

Natumai ni wazima na mnaendelea vyema na libeneke, wakuu nina swali moja la kizushi naomba mniwekee katika blog zenu:

Kwanini Tume ya Uchaguzi Tanzania imeshindwa kulinda na kuheshimu uhuru wa wapiga kura kwa kuanika wazi majina, tarehe ya kuzaliwa, jinsia ya mpiga kura na anuani za wapigaji kura bila ya kutohofia tupo katika ulimwengu ambao unatisha ambapo majambazi, magaidi, matapeli, n.k wanaweza kutumia hizo details katika kuvunja sheria na kufanya criminal activities zozote zile.

mfano: Gaidi anaweza kuchukua details zote za mpigaji kura na kulipua sehemu na kuacha details za mpigaji kura ili kuonesha huyo mpigaji kura ndie amehusika na tukio ilo la kigaidi ili kuficha nyenendo zake na kutokamatwa na badala yake mpiga kura kuingia ktk matatizo!! Huu ni mfano lakini mengi mabaya yanaweza kutokea kutokana na uzembe wa Tume ya Uchaguzi Tanzania.

Tunaomba Serikali, Tume ya Uchaguzi, na wadau wote wahusika kufikiria mpango mwingine wa kufanya katika chaguzi nyingine na kulinda habari nyeti za wapigaji kura, pia serikali ilinde Privacy za watanzania, mfano nchi nyingine nyingi zina Data Protection Act na zina mlinda mwananchi.

Pia wananchi na Wabunge wenu na wawakilishi wengine waweze kuwalinda na kupeleka muswada huu eidha bungeni au popote pale panapohusika maana mpango wa kuanika Sensitive Information za wapigaji kura zaidi ya milioni 5 ktk kila vituo vya kupigia kura (ushaidi upo) ni hatari na kinyume cha sheria!!

Nashukuru.
Mtanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad