
Asalaam Aleykum, Wasomaji wote wa globo hii
Baada ya Salaam, sisi ndugu zenu wa Leeds tunawapa mkono wa EID na kuwaombea afya njema furaha na amani katika kusherehekea sikukuu hii ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani, Sisi wakazi wa Leeds tumesherehekea kwa kuswali swala maalum ya EID iliyofanyika saa mbili asubuhi, Lincoln Green Mosque LS 9 LEEDS na kisha kupata futari ya pamoja katika ukumbi wa MABGATE.
Tunamuomba Allah, atupokelee funga zetu, awajaalie kila lenye heri duniani na kesho akhera
Wabilah Taufiq
Asalaam Aleykum
Mwenyekiti Amran Rashid na Sheirk Mahir Muandazi
No comments:
Post a Comment