
Na Ripota Wa Mtaa Kwa Mtaa Blog.
JAMII na mamlaka husika zimetakiwa kuchukua hatua ya haraka ya kuhakikisha inawalinda watoto ilikuepuka matatizo mbalimbali ikiwemo vitendo vya kilaghai na ukatili vinavyofanywa na watu wasio jali hutu wa watoto.
Akiongea na Mwanahabari wa Blogu hii jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea Haki za Watoto nchini, Nimka Lameck (11) alisema kipindi hichi kumekuwapo na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wadogo huku jamii ikinyamaza.
Nimka alizitaka mamlaka kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuwalinda watoto waliohitimu elimu ya shule za msingi hivi karibuni hususan watoto wa kike ambao kwa asilimia kubwa wapo hatarini kushawishika na walaghai hao maafu kama ‘Mafataki’.
“Watoto wanahitaji kuangaliwa kwa umakini na kulindwa kuepuka matatizo ya kutendewa mahovu kwa jamii isiyo na hutu wa watoto wadogo ambao wanakatisha ustawi wa watoto nchini” alisema Nimka.
Alitoa wito kwa wazazi kuwa na mwamko wa kuchunguza mienendo ya watoto wao mara kwa mara ikiwemo kuwakataza tabia hatarishi ambazo wanaweza kukumbana nazo kipindi wawapo majumbani.
Katika hatua nyingine, Nimka alikemea na kurahani vitendo vya kikatili vilivyolipotiwa kwenye vyombo vya habari juu ya watoto wadogo kuuwawa kikatili ikiwemo na kubakwa vilivyofanywa na watu wazima.
“Vitendo vilivyolipotiwa vimesikitisha,vimetikisa watoto wengi si wa Tanzania tu, bali hata dunianikote kwani watoto waliotendewa unyama huo walikuwa hawana hatia tunaomba sheria kali dhidi ya wahusika” alisema Nimka.
Aidha, alisema kwa sasa yupo katika hatua ya mwisho kuandaa mpango maalum juu ya kutoa changamoto kwa watoto hapa nchini utakaoitwa ‘Haki Mtoto’.
No comments:
Post a Comment