HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 14, 2010

msimu wa nondozz ughaibuni sasa umewadia

Ndugu wadau,

Napenda kuwakumbusha tu kwa wale ambao wana nia na mipango ya kusoma ughaibuni kwa kupata udhamini toka katika vyuo husika au serikali za nchi husika, huu ndio muda wa application. Kwa wanafunzi wa kimataifa, mfano kutoka Tanzania kuja kusoma Marekani, Ulaya nk muda wa ku-apply huanza September – December kwa niaba ya kuanza mwaka mpya wa masomo wa August 2011.

Ili kuweza kupata udhamini huo, ni vyema mtu ujipange na kuzifuatilia habari hizi za scholarships kwa makini mno. Wiki hii nime-post scholarships information nyingi kwenye Scholarship Forum yangu www.scholarshipnetwork.ning.com na Makulilo Blog www.makulilo.blogspot.com. Nakushauri ujiunge uwe member wa Scholarship Forum hiyo ili uweze kuwa unapata scholarship updates kwenye e-mail yako kila mara ninapoweka nondozi mpya huko.

Kwa sasa nipo katika maandalizi ya kuanzisha Makulilo Foundation www.makulilofoundation.org ambayo inakwenda sambamba na utunzi wa kitabu SCHOLARSHIPS IN AMERICA AND EUROPE: The Secrete From Makulilo, Jr. na pia uanzishaji wa The Ernest Makulilo Peace Scholarship ambayo itasaidia mwanafunzi mmoja kila mwaka kuanzia August 2012 kuja kusoma MA Peace and Justice katika University of San Diego, hapa California.

Nawatakia mafanikio mema.

Kama una swali niandikie hapa makulilo@makulilofoundation.org

MAKULILO, Jr.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad