HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 12, 2010

kocha mpya wa timu ya taifa ya mchezo wa pool atambulishwa leo

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa pool Tanzania (TAPA),Isack Togocho (kati) akizungumza leo wakati wa utambulisho wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Pool,Denis Lungu (kushoto) toka nchini Zambia.kulia ni Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa Pool Tanzania (TAPA),Amos Kafwinga.
Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Pool,Denis Lungu toka nchini Zambia akiongoe na wanahabari (hawapo pichani) waliofika katika hafla ya utambulisho wake leo katika kijiji cha Makumbusho,Kijitonyama.kulia ni Mwenyekiti wa chama cha Pool Tanzania,Isack Togocho na kushoto ni Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Zambia nchini,Sunday Chikoti. baadhi ya wanahabari waliofika leo katika hafla ya utambulisho wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya mchezo wa Pool.
Mdau mkuu wa Pool,Bw. Innocent Melleck (shoto) akipena mkono na Kocha mpya wa timu ya Taifa ya mchezo huo,,Bw. Denis Lungu (pili toka kushoto).wengine pichani toka upande wa kulia ni Katibu mkuu wa mchezo wa Pool Tanzania,Bw.Amos Kafwinga,Meneja wa Kocha mpya wa timu ya Taifa,Bw. Stanlas Chisanga,Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Zambia nchini,Bw. Sunday Chikoti mara baada ya hala ya utambulisho wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Pool uliofanyika leo katika kijiji cha Makumbusho.

*********************************************
*********************************************
Chama cha mchezo wa Pool Tanzania (TANZANIA POOL ASSOCIATION- TAPA) kwa kushirikiana na mdhamini mkuu wa chezo huo wa pool nchini Bia ya Safari Lager, inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imemtambulisha rasmi kocha mpya wa timu ya taifa ya mchezo huo kutina nchini Zambia,Bw. Denis Lungu kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia tarehe 01.08.2010 mpaka 28.07.2012.

Lengo la kumleta kocha huyu ni kama inavyoeleza katika katiba kuwa chama kitasimamia na kuendeleza mchezo wa pool table Tanzania na kwa kuzingatia jukumu hilo zito, Chama cha Pool Tanzania kwa kushirikiana na mdhamini wao mkuu wa mchezo wa pool table nchi,Safari Lager waliamua kumleta kocha huyo ili kuhakikisha kwamba mchezo unachezwa katika kiwango cha juu hapa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu mkuu wa chama cha pool Tanzania,Bw. Amos Kafwinga alisema “Ni azma ya Chama cha Pool Tanzania kuhakikisha mchezo unachezwa kwa kufuata sheria na viwango vinavyoeleweka ili mchezo uwe na ladha na hata mtazamaji afurahie kuangalia ili kutekeleza vyema hazma ya mdhamini wetu Safari lager ya kuleta mapinduzi ya kweli na mafanikio makubwa katika mchezo wa Pool hapa nchini.


Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA),Bw. Isack Togocho amewasihi wachezaji wa timu ya Taifa na watakao teuliwa katika timu ya taifa wamtumie vyema kocha huyu ili kukuza viwango vyao na hatimaye waweze kupata nafasi ya kusajiliwa katika vilabu vya kulipwa nje ya nchi. Pia aliwaasa sana wale wote watakaopata bahati ya kufanyan kazi na kocha huyo katika kipindi atakachokuwa nafundisha watumie nafasi hiyo vizuri kwani ni nadra sana kurudi tena.

Mwisho, kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA),Bw. Isack Togocho alitoa shukrani zake za dhati kwa Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kwa mchango wake wa dhati kwa mchezo huo kwa kusema,”Tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa bia ya Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa mchango wao katika kuhakikisha mchezo huu wa Pool unakuwa na kupata hadhi ya juu hapa nchini na kumpongeza sana meneja wa Bia ya Safari Lager Ndugu Fimbo Butallah kwa kuwa bega kwa bega na mchezo wa pool Tanzania.

Kwa kweli TBL kupitia BIA yake ya SAFARI LAGER wamekuwa Ni mfano mzuri katika udhamini Kwa kutekeleza ahadi Na kutoa ushirikiano mkubwa katika mchezo huu, na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad