HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 13, 2010

Mzee Wa Miaka 99 Alamba Nondozz

Akasease Kofi Boakye Yiadom

ana miaka 99 hivi sasa, alipigana Vita Kuu ya Pili ya dunia. Kwa mara nyingine tena Akasease ameushangaza ulimwengu. Akiwa na umri wa miaka 99 kibindoni amehitimu shahada yake katika Chuo Kikuu huko nchini Ghana.

Akasease ni mwalimu mstaafu kitaaluma, akiongea na televisheni ya CNN amesema, "Kama akili yako bado ina uwezo ni poa, kama macho yako bado yanaona ni safi sana, kwa sababu ukienda shuleni bado utaweza kujifunza."

Baada ya kuhitimu shahada yake Akasease amekuwa akiwahimiza wahitimu wenzake kutokimbilia ulaya kwa sababu ya mshahara mzuri, bali kubaki nyumbani na kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Juhudi za Akasease zinaonekana kuzaa matunda kwani wengi ya wahitimu wa nchini Ghana kwa sasa wanaonekana hawana mzuka sana wa kukimbilia nje nchi kwa ajili ya ajira.

Kinyume chake ni kwamba wengi ya wahitimu wa nchini Ghana, hata wale wanaosoma katika vyuo vya ughaibuni, wanaonekana kurudi nyumbani kwa kasi.

Taasis ya International Organization for Migration (IOM) imesema kuanzia mwaka 2000 hadi 2007 Waghana zaidi ya milioni walikimbilia ughaibuni lakini karibu asilimia 85 ya hao wamerejea nyumbani ama moja wa moja au japo kwa muda mfupi.

Msemaji wa taasis ya IOM amesema sekta inayoathirika zaidi kutokana na Waghana kukimbilia ughibuni ni ile ya afya, "Miaka ya mwanzoni ya 2000 kulikuwa na wilaya nyingi ambazo hazikuwa na daktari, na kuna wadi kadhaa za hospitali ambazo hazikuwa na nesi hata mmoja. Hii ilisababisha idadi ya vifo vya watoto na mama wajawazito kuwa juu sana".

Bob Sankofa
fotobaraza.ning.com
wahapahapa.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad