===================================
SAMSUNG Miss Tanzania India yazinduliwa rasmi.
Richa Adhia kuwakilisha TANZANIA
Uwakilishaji wa TANZANIA kwa mara ya kwanza kwenye 19th MISS INDIA WORLDWIDE
Samsung Miss Tanzania India imezinduliwa jana usiku kwa tafrija iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar-es-Salaam.
Miss Tanzania India ni jukwaa linalotoa fursa kwa wanawake wa Kitanzania wenye asili ya Kihindi kuweza kushindana kuonyesha urembo na vipaji vyao ambapo mshindi ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kidunia ya Miss India worldwide.
Ikiwa ni mara ya kwanza, Miss Tanzania India imedhaminiwa na Samsung Electronics, kampuni inayoongoza kwenye nyanja ya mawasiliano duniani na hivyo kufanya ipewe kipaumbele kwa kuliitwa kwa jina la Samsung Miss Tanzania India.
“Mshindi wa Samsung Miss Tanzania India mbali na kuitangaza Tanzania kimataifa pia atajihusisha na shughuli za kijamii ikiwa na pamoja na kuchangisha fedha zitazotumika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya Kitanzania” alisema Bi. Sati Gadhvi msemaji mkuu wa Miss Tanzania India.
“Mwaka huu ikiwa ni mara ya 19 kwa mashindano ya Miss India Worldwide yatakayofanyika tarehe 27 Machi 2010 kwenye ukumbi wa International Convention Centre mjini Durban, Afrika Kusini. Mrembo Richa Adhia ataipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mashindano hayo” aliongezea Bi. Gadhvi.
Uzinduzi wa Samsung Miss Tanzania India umeenda sambamba na kusheherekea siku ya Wanawake duniani kwa tafrija ya “Bollywood Party” pamoja na DJ maarufu kutoka jijini Mumbai nchini India DJ JULZ.
“Sisi kama Samsung tumeona kuna umuhimu wa kuunga mkono shughuli za maendeleo ya wanawake. Miss Tanzania India imeandaa jukwaa maridhawa kwa kuweza kujadili mambo mbalimbali ya kijamii na kutatua matatizo yatakayoelekea kuboresha maisha ya jamii husika na kuhamasisha vijana kukabiliana na matatizo mbalimbali .
Hii si kwa ajili ya urembo tu bali pia kuboresha mwonekano maridhawa inayoelekea kwa Samsung kuwa na bidhaa zinazoongoza kwenye nyanja za mawasiliano” amesema Simon Kiriithi, Meneja wa Samsung Tanzania.
“Uzinduzi wa Samsung Miss Tanzania India Inaenda sambamba na kusherehekea siku ya wanawake duniani” Alihitimisha Bi. Gadhvi
Kuhusu SAMSUNG Miss Tanzania India
Miss Tanzania India ni jukwa linalotoa fursa kwa wanawake wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kuweza kushindana kuonyesha Urembo na Vipaji vyao ambapo mshindi atavikwa taji na kuiwakilisha Tanzania kwenye fainali za Kidunia za Miss India Worldwide
Shughuli hiyo yameandaliwa kusherehekea urembo na sanaa Kutoka bara la Hindi na kulipatia Mrembo Mtanzania mwenye asilia ya Kihindi kuitangaza Tanzania kimataifa na kujihusisha na shughuli za kijamii ikiwa pamoja na kuchangisha fedha zitazotumika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya Kitanzania.
Samsung Miss Tanzania India ni wakala rasmi was mashindano ya kimataifa ya Miss India Worldwide nchini Tanzania
Kuhusu Samsung Electronics Co., Ltd.
Samsung Electronics Co., Ltd. ni kampuni inayoongoza duniani katika Nyanja ya technologia na mawasiliano ikiwa na rekodi ya mauzo ya dola za kimarekani 96 billioni ikiwa sawa na 12.96 trillioni kwa pesa za Kitanzania mwaka wa 2008. Inajumla ya waajiriwa 164,600 kwenye ofisi 176 katika nchi 61 duniani.

Kampuni ya Samsung ina biashara saba tofauti zinazojitegemea ikiwa pamoja na Visual Display, Mobile Communications, Telecommunication Systems, Digital Appliances, IT Solutions, Semiconductor na LCD.
Imetambulika kama ni kampuni inayokua haraka duniani , Samsung electronics inaongoza kwa kutengeneza digital TVs, memory chips, mobile phones na TFT-LCDs.
Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti www.samsung.com
Kuhusu Richa Adhia
Richa Adhia alizaliwa jijini Mwanza, na amekua akijihusisha na shughuli za uanamitindo tangu mwaka 2003 alipogunduliwa na Mustafa Hassanali. Aliiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya fainali za “Miss Earth”nchini Ufilipino mwaka 2006 na baadae kuwa Vodacom Miss Tanzania mwaka 2007 ambapo alipata fursa ya kuiwakilisha Tanzania kwenye fainali za kumtafuta mrembo wa dunia “Miss World” mjini Sanya nchini China.
Richa sasa ni mjasiriamali anayemiliki saluni ya urembo iitwayo Radiance, iliyopo Upanga jijini Dar-es-Salaam na ataiwakilisha Tanzania tarehe 27 Machi 2010 kwenye fainali za Miss India Worldwide nchini Afrika Kusini.
TOVUTI: www.misstanzaniaindia.com
No comments:
Post a Comment