
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam William Lukuvi akihutubiwa wanawake na wakazi wa jiji la Dar es salaam katika viwanja vya mnazi mmoja leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika leo Duniani kote, nchini Tanzania siku hiyo imeadhimishwa kitaifa Mkoani Tabora ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Wanafunzi wakike kutoa shule mbalimbali wakiwa wameshika bango lenye ujumbe wa unaoelezea miaka 15 ya mafanikio ya wanawake baada ya mkutano wa kimataifa uliofanyika Beijing nchini China.

Wanawake kutoka Wizara ya Mambo ya ndani kitengo cha malalamiko wakipita na bongo lao mbele ya mgeni rasmi.

Brass Band ya Magereza ikiongoza maandamano ya Wanawake wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam na wakati kitaifa yamefanyika mkoani Tabora,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.Picha na mdau John Bukuku wa Full Shangwe Blog.
No comments:
Post a Comment