HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 6, 2010

Kamzinga Kakiaina Katika Kivuko Cha Mv Magogoni Leo

hiyo canter inyoonekana hapo ilifeli breki wakati ikitoka katika kivuko cha Mv. Magogoni na kurudi nyuma kwa spidi mpaka kuigonga hiyo pikup nyingine hapo kwa nyuma nayo ikagonga nyingine.kambonyeo kakiaina huku dereva wake akiangalia kwa huruma.
mashuhuda kama kawa na yule mwenye pikup nyingine ilibidi aondoke zake maana gari yake haikuumi sana.
ilibidi ije hii fuso kutoa msaada wa kuivuka hiyo Canter iliposhindwa kupanda tena kwa mara nyingine hicho kilima cha kivukoni.katika ajali hii hakukuwa na mtu yeyote alieumia ila ni magari tu.sasa sijui huyu jamaa watamchukulia hatua gani maana pia alipakia mzigo wa chokaa ambayo hairuhusiwi katika kivuko chochote kile hapo.

1 comment:

  1. inaelekea mzigo ulizidi vinginevyo break haifeli labda gari break zake ni mbovu au pia dereva ana leseni uchwara

    ReplyDelete

Post Bottom Ad