Watafiti wa mambo ya teknolojia huko Uingereza wanapiga kazi usiku na mchana kuhakikisha ndani ya muda mfupi tangu sasa utakuwa huna haja ya kubeba simu yako ya mkononi wala kutumia kompyuta kufanya mawasiliano ya intaneti.Watafiti hawa wanasema teknolojia wanayoilalia mlango wazi itakuwezesha kufanya shughuli zako za kimtandano na burudani zote kwa kutumia ngozi ya mwili wako kama simu au kompyuta.
Wenyewe wanasema wamekuja na teknolojia hii ili kuwapunguzia binadamu mizigo wanayojibebesha kila wanapokwenda makazini na pia kupunguza idadi ya mavituvitu ndani ya makazi yako.
Tafadhali tazama video hii kuelewa kwa undani jamaa wanasema nini.
imeletwa na Mdau
Babukadja
wa
http://fotobaraza.ning.com
No comments:
Post a Comment