HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 12, 2010

Miss Tz 2009/10 Apandishwa Kizimba Leo

Mrembo Miriam Gerald na rafikiye Kenedy Vicror wakipelekwa mahabusu baada ya kesi yao kuahirichwa mpaka Februari 25,2010
watuhumiwa Miriam Gerald na rafikiye Kenedy Victor wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wakisomewa mashtaka mapema leo asubuhi.kesi yao imeahirishwa mpaka Februari 25.picha kwa hisani ya Father Kidevu Blog
miss Tanzania 2009/10 Miriam Gerald akiwa katika pozi

Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald na Boyfriend wake Kenedy wamepandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akishitakiwa kwa kosa la kufanya vurugu na kuharibu mali za bendi ya muziki ya Volcano Sound inayomilikiwa na mwanamuziki Taji Mbaraka Mwishehe,mtoto wa Marehemu Mbaraka Mwishehe kwenye ukumbi wa TPDC Mikocheni.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Oysterbay na ilikuwa na jalada na OB /RB/2267/010 KUHARIBU MALI NA SHAMBULIO imesomwa leo katika mahakama hiyo na mshitakiwa Miss Tz Miriam Gerald.

Miriam amewekwa mahabusu ya mahakama hiyo baada ya kukosa dhamana, kesi imaeahirishwa, hata hivyo ndugu na jamaa wa mrembo huyo wanahangaika ili kuhakikisha anapata dhamana kabla muda wa kuwachukua mahabusu kutimia ili kuweza kumnasua mrembo huyo ili asipelekwe rumande, bado haijafahamika kama masharti yote ya dhamana yataweza kutimia leo au la.

Kimsingi kama Miriam atapatikana na hatia hii itakuwa ni jambo baya kwa mrembo huyo anayeshilikila taji la Miss Tanzania 2009/2010 kwakuwa mrembo huyo aliaswa na wadau mbalimbali wa urembo kuwa balozi mwema kwa Nchi, jamii na kwa kamati ya Miss Tanzania.

tunawatafuwa viongozi wa Kamti ya Miss Tanzania ili tuweze kusikia maoni yao juu ya jambo hili lililomkuta mrembo wao huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad