HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 12, 2010

SHINDA ZAWADI KIBAO NA WWW.WAHAPAHAPA.COM


Shiriki ujishindie moja ya zawadi kumi za muda wa maongezi wa TSHs. 5000/- kila wikina mizawadi mingine kemkem, kila wiki, kwa kushiriki shindano katika tovuti yako penzi ya Wahapahapa. Unachotakiwa kufanya ni kuangalia "Wazo la Mwezi (theme)" na kutuma picha ama insha inayoendana na wazo hilo. Zawadi zingine ni kama T-shirt za Wahapahapa, Kaseti au DVD za mchezo wa radio wa Wahapahapa, na posta kali za Wahapahapa. Pia kuna zawadi kubwa kila mwisho wa mwezi inayokwenda kwa jina la "Furushi la Wahapahapa" ambapo mshindi anapata zawadi zaidi ya moja kwa mkupuo.

1. MAELEZO SHINDANO LA PICHA


Picha iwe na maudhui ya "Wazo la Mwezi (theme)" Piga picha yako na kuituma ikiambatana na maelezo ya mahala na siku picha ilipopigwa. Picha iwe ya kiwango cha kuridhisha ili iweze kuingia kwenye tatu bora. Picha zitakazotumwa zitaingizwa katika mchujo na timu ya uendeshaji wa tovuti itachagua picha tatu kali (uamuzi wa majaji ni wa mwisho), halafu zitapigiwa kura na wadau wa tovuti, katika tovuti, ili kumpata mshindi atakayeserebuka na zawadi. Kutakuwa na washindi watano wa muda wa maongezi kila mwisho wa wiki. Pia kutakuwa na mshindi mmoja kila mwezi atakayejishindia "Furushi la Wahapahapa". Picha itakayonyakua zawadi itawekwa ukurasa wa mbele wa tovuti ya Wahapahapa.

2. MAELEZO SHINDANO LA INSHA


Insha iwe na maudhui ya "Wazo la Mwezi (theme)", halafu unaituma kwenda wahapahapatz@gmail.com. Picha yako ikiambatana na picha itapendeza zaidi. Insha isizidi maneno 300 na isipungue maneno 150 yaliyochapwa kwa tarakilishi (kompyuta), na iwe ya kiwango cha juu ili iweze kuingia kwenye tatu bora.
Insha zitakazotumwa zitaingizwa katika mchujo na timu ya uendeshaji wa tovuti itachagua picha tatu kali (uamuzi wa majaji ni wa mwisho), halafu zitapigiwa kura na wadau wa tovuti, katika tovuti, ili kumpata mshindi atakayeserebuka na zawadi.

Kutakuwa na washindi watano wa muda wa maongezi kila mwisho wa wiki. Pia kutakuwa na mshindi mmoja kila mwezi atakayejishindia "Furushi la Wahapahapa".
Insha itakayonyakua zawadi itawekwa ukurasa wa mbele wa tovuti ya Wahapahapa.

Muda wa Shindano hili ni;


Zawadi: Muda wa maongezi ya simu ya TSHs. 5000/-
Pia utume nambari ya simu na anuani ya posta ili zawadi zako zikufikie kirahisi. Nambari na anuani ni kwa matumizi ya shindano pekee na si vinginevyo.

Web Administrator

www.wahapahapa.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad