
bwana harusi Bahati Singh na bi Harusi Zenat Singh wakiwa katika furaha ya ndoa yao.

bwana harusi na mkewe wanaelekea sehemu yao maalumu waliotengewa jioni hii,wakijumuika pamoja na wageni waalikwa waliohudhulia hafla hiyo

bwana harusi na wapambe wake wakikaa mkao wa kula solo la manyamanyama

bwana harusi na bi harusi wakiwa katika picha ya pamoja na Mama mzazi wa bibi harusi

bwana harusi,Bahati Singh pamoja na mkewe Zenat wakiwa na wageni wao waliofika katika hafla yao hiyo iliyomalizika jioni hii huko Mbezi beach.


wafanyakazi wenzake na bwana harusi wakifuatilia shughuli kwa makini.

mambo ya mduariko nayo hayakuwa nyuma kwa upande wa kina dada.leo mdau Bahati Singh ambaye ni Meneja Matukio na Promosheni wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) aliamua kuukacha rasmi ukapera na kuamua kufunga ndoa mapema na mkewe bi Zenat,ambapo hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa bwana harusi huko Mbezi Beach na mambo ndio yalikuwa kama yanavyoonekana katika picha hizi
.
No comments:
Post a Comment