HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 15, 2010

Mambo Ya Valentine Dei Na Acudo Impact

Malkia wa Acudo Impact,bibie Emirod akiwajibika stejini.bibie huyu alinitonya kuwa anakaribia kuporimosha albamu yake matata sana ambayo ndani yake kuna vichwa matata kama vile Mzee King Kikii na Banana Zoro pamoja na wengine ambao hakunitajia.na anasema siku si nyingi kitu kitaanza kusikika,hivyo kaeni mkao wa kula.
mpiga kinanda maarufu sana hapa bongo,Andrew Segedia akiwajibika ipasavyo.
jukwaa la Msasani Beach lilivyokuwa kwa siku ya jana ambayo ilikuwa ni maalumu kwa wapendao kama mimi na yule.
Toto ze Bingwa akipuliza tarumbeta ikiwa ni moja staile yao ya sasa.
Mh.Kapuya nae hakutaka kupitwa na vitu vikali toka kwa Vijana wa Masauti,ilibidi azame kati kulisakata rumba.
juu ni wacheza shoo wakiume na chini ni wakike wakikamilisha siku zao katika kazi na staili yao ya kibajaj
wapenzi wa Acudo wakilisaka rumba kisawasawa katika wanja la Msasani Beach club usiku wa kuamkia leo,ambapo palikuwa hapatoshi kwa jinsi kulivyoshona.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad