HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 8, 2010

Mada Ya Msingi

Habari Kijana wa Mtaa Kwa Mtaa,

hebu weka haka ka mada hapa mtaani wadau wakachangie.
Katika mambo mimi yananikera Tanzania hii ni kuona mtu aliyeua jambazi anaonyeshwa hadharani lakini jambazi lililowawa au kukamatwa au kukimbia kwamba linatafutwa halionyweshwi. Sasa namna hii tutamaliza ujaambazi namna gani?.

Kwa nini mtu jambazi anakamatwa lakini tunaonyweshwa silaha peke yake?. Kwa nini tusionyeshwe Jambazi lenyewe ili sisi Raia wema tusaidie Polisi kuwataja watu walio na mahusiano na Jambazi huyo. Mimi naona ni makosa kumuonyesha Askari aliyeua Majambazi kwani tunamhatarishia usalama wake.

Anayepaswa aonyeshwe hadharani ni Jambazi ili watu waweze kuwataja watu wenye mahusiano ya ujambazi au ya biashara na mtu yule. Jeshi la Polisi naombeni badilini utaratibu wenu wa kuficha sura za wahalifu. Itasaidia kupunguza uhalifu kama mtaweka wazi sura za watu hawa.

Sioni kama utaratibu wa sasa wa kuonyesha aliyeua jambazi ni sahihi. Aliyeua umeshamzawadia yeye hataki sifa kuonyeshwa kwenye magazeti kwani kunamletea hali hatarishi kwa usalama wake na familia yake.

Mdau Mzalendo.

4 comments:

  1. Make soooooo much sense. Ndio maana watu hawataki hata kwenda kuchukua zawadi zao kwani kuna kupata pesa uykakosa familia na maisha yako kwa ujumla. Majambazi ya home yanafanya kazi kwa kushirikiana na kwa kumuonesha aliyeua unakuwa unahamasisha revenge kwa msaidizi wa jamii
    Aliyetoa mada namuunga mkono na nakuomba Kaka Othman niipeleke kule kijiweni nako wanaotembelea wajiulize.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Mzee wa Changamoto kumbe umeliona hili eehh?? basi hivi ndivyo mambo yanavyokwenda hapa kwetu yaani majambazi kila siku tunawasikia kwenye bomba tu kuwa wamekufa lakini hatuwaoni zaidi ya kuonyeshwa silaha tuu.sasa kwa mpango huu tunawatengenezea nini hawa askari wanaofanya kazi hiyoooo??????

    Mdau Mzalendo.

    ReplyDelete
  3. hii imekaa sawa hata mimi nilifikiri hivyo kwanza kwa askari muuaji sijui ataonekana vipi ktk jammii yake zaidi ya muuaji/mkatili, na hapati mume hapo

    pia usalama wa askari ni wamatata sana hawa jamaa huwa wanamitandao mikubwa watamtafuta na watampata

    ReplyDelete

Post Bottom Ad