Akiwa Ottawa Mhe. Waziri Membe atapenda kukutana na Watanzania waliokoCanada. Ubalozi unafanya utaratibu wa kupata ukumbi kwa ajili yamkutano huo ambao utafanyika siku ya tarehe 12, Januari, 2010 jionisaa Kumi na Mbili na Nusu hadi saa Tatu na Nusu usiku (6:30Pm-9:30Pm).
Tutawajulisha sehemu ya mkutano na anuwani ya shughuli hiyo kabla ya mwisho wa juma hili hivyo tunaomba muweke shughuli hii katika ratiba
zenu.
Aidha, tunaomba kila atayepata ujumbe huu atusaidie kumjulisha/
kuwajulisha Watanzania wenzetu ambao hatukuweza kuwatumia
barua pepe hii kutokana na kutokuwa na anuwani zao.
Kama mnavyojua shughuli ni watu na watu ndiyo sisi sote hivyo tunaombatujitokeze kwa wingi kuja kukutana na Mhe. Waziri Membe ambaye kama wengi mnavyokumbuka aliishi hapa Ottawa wakati akifanya kazi kwenye
Ubalozi wetu huu.
Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu,
Changamkeni acheni uzembe oneni wenzenu UK na USA, Abdallah Mwailubi,Calgary.
ReplyDelete