HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 13, 2010

King Kif Nae Amwaga Cheche Zake

Habari zenu wana blog wenzangu!
Nikiwa mmoja ya wanablog kutoka www.kingkif.blogspot.com kwa kupitia blogu hii naomba nichangie japo kwa aya machache kuhusu ukumbe wa Kajuna son wa kijiji cha Habari na Matukio (
www.kajunason.blogspot.com) ambapo mapema mwezi huu aliandika kwenye blogu mbalimbali .Hivyo basi , na mimi King Kif napenda kushare hili na ndugu zetu ili walifahamu hili.


Tangu nimeanza kublogu nina muda wa miezi tisa sasa ! Ni muda mfupi mno! Lakini kwenye muda huo kiduchu nimeweza kupokea e.mail nyingi sana kutoka hapa Tanzania na nnje ya nchi ambazo watu wanaomba niwatangazie mambo yao kupitia blogu yangu na nyingineziliomba niwatumie hata wamiliki wa blogu nyingine ambao ni marafiki zangu!Kwa bahati mbaya ama kwa makusudi mazima ni ni wachache sana ambao wanajua umuhimu wa kurudisha fadhila au hata kutuma mialiko ya matukio ambayo wanayafanya(hasa hapa Tanzania).

Hapa kwenye aya hii ninamnukuu Kajunason: "Jambo baya na la kusikitisha kabisa hawa watu pale unapopata nafasi ya kwenda utaambiwa hautambuliki kabisa kwa nini nisitambulike wakati unanitumia e.mail ili nikutangazie mambo yako ulinitambuaje? na leo nimekuja kwenye hicho kitu kuangalia kama kweli kimefanyika unasema haunitambui?".


Washiriki wenzetu , nimeamua kuandika e.mail hii ili kuweza kusema ukweli...haiwezekani ukanitumia tangazo au matangazo na kuomba utangaziwe concert, upigaji mnada , au tukio lolote harafu hautumi mwaliko inakuwa haina maana ninaomba tubadilike huu ni mwaka mpya 2010.


Ni mimi,
Kingkif wa
www.kingkif.blogspot.com
...ustarabu ...ni jambo jema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad