HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 29, 2009

Maoni Ya Master T Kwa Wana Blogu

Salaam kwako Kaka na Wote!

Nimefurahi na kuguswa sana na waraka wa Mwana Changamoto!
Nipo tayari kushiriki kikamilifu katika azimio lolote litakalokubaliwa. Nitahamasisha jamii ya wana Umodo tujitolee kusaidia jamaa zetu walio katika mazingira magumu.

Kuna eneo moja la msingi ninaloliwaza, nalo ni Utawala Bora. Nisingependa kushawishi fikra za kisiasa hapa lakini natoa oni tu kwamba bila kuzingatia Utawala na kushinikiza watawala wetu kuwajibika zaidi, tutajikuta tunarudia sana shughuli za kusaidia wahanga wa utawala hola!!

Sasa, naafiki bloggers wa Tanzania tutoe mchango wetu kwa "masikini" lakini pia tufikishe ujumbe wetu kwa njia za ubunifu kwa viongozi wetu kwamba hawafanyi ya kutosha kumfikia mwananchi wa kawaida mwenye maisha ya kawaida na mwenye mahitaji ya kawaida.

Eh, nimeanza kuchepuka! Point ni kwamba kuandika katika forums tetesi za ufisadi na kufichua memo za siri haitoshi, citizen journalist anaweza kuwa na impact zaidi kwa kubuni suluhu za matatizo ya kweli, mbinu za hakika na maarifa makini ya kumkomboa Mtanzania asiye na "empowerment' kama yetu sisi tunaosoma haya!

Kama sijaeleweka, dah, ni kawaida yangu kutojieleza vizuri na kiswahili changu kibovu.
Pamoja.

Taji a.k.a Master T

Gonga Hapo Ukaone mambo yake

http://modotz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad