
dereva wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika jina lake kwa mara moja akijaribu kutoka kwenye gari hiyo mara baada ya wasamalia wema kufanikiwa kulipindua ili kumsadia ndugu huyu.

dereva wa gari hiyo aina ya toyota Corrona lenye nambari za usajiri T933APF akitoa kichwa nje mara tu baada ya gari hilo kupinduliwa ili aweze kutoka maana lililala kabisi kichwa chuni miguu juu baada kupinduka asubuhi ya leo maeneo ya Ubungo stendi ya mkoani,lilipochomekewa na daladala wakati gari hii iko katika mwendo wa kasi sana.

wasamaria wema wakijitahidi kulipindua gari hili kutoka mtaroni ili kuweza kumtoa dereva wa gari hiyo ambaye inaonekena aliumia sana baada ya gari hilo kupindukia mtaroni asubuhi ya leo katika maeneo ya Ubungo stendi ya mkoani.

wasamalia wema wakihangaika kulinyanyua gari hilo
watu kibao walifika kushangaa kwanza kilichotokea kabla ya kuanza kutoa msaada mara tu baada ya kutikea ajali hiyo leo asubuhi maeneo ya Ubungo stendi ya mkoani.
No comments:
Post a Comment