Watangazaji kutoka wa Clouds Fm Ephraim Kibonde (magazetini jahazi) pamoja na Gerald Hando ( Power breakfast) wakirusha live mchakato mzima wa shindano hilo,ambalo wadhamini wakuu walikuwa ni kampuni ya simu ya Zain pamoja na kampuni ya bia ya Serengeti wakiwemo na Nokia Connecting people.
Kituo cha st Piter ambapo washiriki wa Fiesta mikokoteni marathon ilikuwa ni kama kituo cha cha mwisho ambapo kila mmoja alitakiwa kumbeba baunsa mmoja mpaka mwisho wa safari yake.
washkaji wakichanja mbuga kuelekea viwanja vya Lidaz klabu.
ndinga zikiwa sailensi kwaajili ya kupooza injini baada ya kupiga msele mmoja mkali sana
Washiriki wa shindano la Fiesta Mikokoteni Maraton wakiwa wamepozi kwa pamoja leo jioni viwanja vya lidaz club,ambapo mshindi wa nne mpaka wa kumi walipewa kifuta jasho cha shilingi elfu ishirini.
Hapa wakiwa wamekula shavu la tshet za Nokia ambao pia ni moja ya wadhamini wa tamasha la Fiesta Onel 2009 ambalo litafanyika wiki ijayo katika viwanja vya Posta,kijitonyama jijini dar.
Sunday, November 1, 2009

Home
Unlabelled
Fiesta One Love Mkokoteni Marathoni 2009 Ilivyofana Leo
Fiesta One Love Mkokoteni Marathoni 2009 Ilivyofana Leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment