HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 1, 2009

Washiriki Wa Fiesta One Love Mkokoteni Marathoni 2009 Wakipewa Zawadi Zao

Msimamizi wa Mashindano ya Fiesta Mkokoteni Marathoni 2009,Cathbert Angelo Kajuna wa Prime Time Promotions/Clouds Fm ambao ni waandaaji wa Fiesta One Love 2009 akitangaza washindi wa mbio hizo za Mkokoteni Marathoni katika viwanja vya Lidaz Klabu mchana wa leo.
Washindi wa tatu nao wakipata zawadi zao toka kwa Nokia.
washindi wa pili wa Mkokoteni Marathon Edger Mongi (kulia ) na Mohamed Ramadhan (kati) wakipokea zawadi zao toka kwa David Mugutu Wa Nokia.
David Mugutu akiwa na washindi wa kwanza wa Mkokoteni Marathon ndugu Paul silvester na Mathias Mwakipesile wote ni kutoka Namanga Camp,mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao,ambazo ni simu ya mkononi,chupa ya maji pamoja na miwani ya jua kwa kila mmoja.
David Mugutu toka Nokia akionyesha moja ya zawadi watakazozawadiwa washindi wa kwanza wa Mkokoteni Marathon.
washiriki walioingia tatu bora na kuwa washindi wa shindano la Mkokoteni Marathon,wakiwa mbele ya mabango ya Nokia wakipata picha ya pamoja na huku wakisubiria zawadi zao za simu toka Nokia.
Katibu tawala wa wilaya ya kinondoni Mh Patrick Benard akiwakabidhi zawadi ya tshet za Zain na kofia Paulo Silivester na Mathias Mwakipesili kutoka Namanga Camp,ambao ndiyo washindi wa kwanza mbio za mikokoteni marathoni zilizofanyika leo jioni,Camp hiyo pia ilizawadiwa kitita cha shilingi milioni moja..
Katibu tawala wa wilaya ya kinondoni Mh Patrick Benard akiwakabidhi zawadi ya tshet za Zain na kofia kundi la Wagumu Halisi ambao ndiyo washindi wa pili wa mbio za mikokoteni marathoni zilizofanyika leo jioni,Camp hiyo pia ilizawadiwa kitita cha shilingi laki tano keshi.
Katibu tawala wa wilaya ya kinondoni Mh Patrick Benard akiwakabidhi zawadi ya tshet za Zain na kofia kundi la Namanga Camp ambao ndiyo washindi wa tatu wa mbio za mikokoteni marathoni zilizofanyika leo jioni,Camp hiyo pia ilizawadiwa kitita cha shilingi laki tatu keshi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad