
Mara nyingi kila ninapokaa na marafiki ama hata wapita njia huwa hawaachi kuniuliza maswali mengi kuhusiana na kazi ninayofanya, (Uchongaji). Lakini wengine huwa wanakwenda mbali zaidi na kuniuliza najihisi vipi kuwa mwanamke mchongaji katika fani ambayo kwa kitambo sasa imekuwa ikitambulika zaidi kama fani ya wanaume. Mara nyingi huwa natamani kuwapa jibu la jumla, kwamba, “Kama wanawake tunaweza kuwazaa wanaume basi hakuna anachofanya mwanaume mwanamke akishindwe”.
Jibu la namna hii linaweza kuwa tata kwa rafiki zangu wengine, maana wapo marafiki wa kiume wasioamini kwamba kazi yeyote inayoweza kufanywa na mwanaume basi hata mwanamke anaweza, halafu mbaya zaidi wapo marafiki wa kike ambao wamelambishwa sumu ya kuamini kwamba yapo mambo ni kwa ajili ya wanaume pekee.Sasa mara nyingi huwa nakumbana na changamoto hii, na mara karibu zote ili kuthibitisha imani yangu kwa watu wengine, imani ya kwamba anachoweza mwanaume na mwanamke anaweza, huwa inanilazimu kuzungumzia hisia juu ya kazi yangu kwa kumualika muuliza swali kuitalii historia yangu.
Kila ninapozungumzia historia ya kazi yangu, mimi binafsi hujihisi kama ndio ninaipitia mara ya kwanza. Kila wakati najifunza jambo jipya ninapotazama historia yangu.
moja ya kazi za Dada Mwandale
Hadithi yangu ni moja ya hadithi nyingi, tena zinazoshabihiana, za binti anayezaliwa katika nchi ya Tanzania, na pengine katika bara la Afrika. Ni hadithi ambayo mara nyingi huanza na Baraka nyingi lakini zisizokosa vikwazo njiani.Baraka ya kwanza ni kwamba mama aliyenibeba tumboni kwa miezi tisa ni Mmakonde, kwa takwimu za haraka ni wazi kwamba kabila la Wamakonde, wenyeji wa kusini mwa Tanzania, ndio wachongaji wanaofahamika zaidi ndani ya nchi hii. Kwa hivyo, naweza kusema sikuchagua kuwa mchongaji, bali uchongaji ulinichagua.
Nimekulia kijijini kabisa na katika utoto wangu nilizungukwa na familia nyingi za wachongaji, japo wengi kama si wote, walikuwa ni wanaume.Baraka ya pili ni kwamba babu yangu mzaa mama yangu alikuwa ni fundi seremala na pia mchongaji wa vinyago, kwa hivyo nilianza kucheza na vifaa vya uchongaji nikingali binti mdogo kabisa, na kwa bahati nzuri babu yangu alifurahi nilipokwenda kucheza katika karakana yake.endelea huku>>>>
SAFI DADA MWANDALE ONGELA KW AKUPIGA HATUA
ReplyDeleteDADA MWANDALE ALIIPENDA KAZI UCHONGAJI TANGU MDOGO NAO UCHONGAJI UKAMPENDA NA MUNGU AENDELEE KUBARIKI KAZI YA MIKONO YAKE
ReplyDelete