
dada Jackline ambaye ni mmoja kati ya watangazaji wa Mbeya Fm waliotembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Simike,akiwa amewabeba watoto mapacha ambao nao wapo kwenye kituo hicho cha kulelea watoto yatima.

DJ mkali wa KWETU AFRIKA,katika Mbeya Fm Bhuruan Said a.k.a DJ Acrama akiwa amepozi na mmoja wa watoto wa kituo hicho.

mambo ya maakali yakiandaliwa tayari na kina mama wa kituo hicho,waliochuchumaa ni wafanyakazi wa Mbeya Fm,toka shoto ni dada Ambwechriss,mtu mzima Smart Boy,kaka Gwamaka, na dada Jackline

watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima Simike wakiwa wamekaa mkao wa kula baada ya kugaiwa kila na wadau wa Mbeya Fm.kituo hiki cha Simike kina watoto 60 lakini wengine walikuwa wachukuliwa na baadhi ya wasamalia wengine kwa ajili ya kwenda kula sikukuu katika makazi yao,ila watoto waliokuwepo siku hiyo walikuwa ni 32.Mlezi wa kituo hicho hakuwepo kwa hiyo aliacha maagizo kwa wakubwa waliokuwepo pale kwani mlezi huyo alimpeleka mmoja wa watoto hao hospitali aliekuwa akiumwa siku hiyo.kwa picha zaidi mtembelee dada Jackline katika wanja lake kwa kubofya
hapa.
No comments:
Post a Comment