HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 18, 2009

Precision Air Pamoja na Kenya Airways Wafuturisha Leo

bosi mkuu wa Kenya Airways hapa Dar,ndugu Emmanuel Chepkong'a akitoa shukrani kwa wadau waliohudhulia katika Iftar hiyo iliyofanyika katika ukumbi Serengeti katika Hotel ya Paradise All Suite City iliyopo katika jengo la Benjamin W. Mkapa Pension Tower jioni hii
Kaimu Bosi Mkuu wa Precision Air, ndugu Tuntufye Mwambesi nae alitoa shukrani zake kwa wadau waliohudhulia katika Iftal hiyo
Sheikh Abou Mohamed Iddy akitoa daawa kwa waliohudhulia katika Iftal hiyo,iliyofanyika jioni ya leo katika Hotel ya Paradise,pale Benjamin Mkapa Tower.
Wadau kutoka sehemu mbali mbali wakiendelea kupata Ftari
Ftari ilikuwa ni ya kujisevia kama uonavyo katika picha hizi
Ftari ikiendelea kulika
Wadau wakiendelea kupata Ftari iliyoandaliwa na mashirika ya ndege ya Precision Air pamoja na Kenya Airways.
baada ya Ftari kila mtu alitulia kimya kabisa kusikiliza mawili matatu toka kwa waandaaji wa shughuli hiyo.
Sheikh Abou Mohamed akibadilishana mawazo na Meneja wa mauzo wa Precision Air kwa Zanzibar na Dar,Ndugu Ibrahim Bukenya pamoja na Ustaadh(jina lake limenitoka kidogo).
kushoto ni Sheikh Abou Mohamed ambaye ndie alieiongoza vyema shughuli hii kwa dua na ibada ya Magharibi,anaefuata ni Meneja Masoko wa Precision Air,ndugu Ibrahim Bukenya na ustaadh ambaye jina lake limenitoka kidogo,wakiwa katika picha ya pamoja mara tu baada ya kumalizika kwa shughuli nzima ya kufturisha wadau mbali mbali wakiwemo mawakala wa ndege hizo za Precision Air pamoja na Kenya Airways,iyofanyika katika Hotel ya Paradise All Suite City,iliyopo ndani ya mjengo wa Benjamin Mkapa Pension Tower's jioni ya leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad