
sehemu ya iliyoharibika kwa gari zote mbili.

Askari wa usalama Barabarani akisikiliza maelezo ya wahusika wa magari hayo mara baada ya kufumuana jioni ya leo pale makutano ya barabara ya Lumumba na Uhuru rodi(mnazi mmoja)

Dereva wa lori akitafakari jinsi ya kumuingia mdosi wake mara baada ya kupata ajari ya kuifumua vilivyo daladala.

mashahidi nao kama kawa.

hizi ndinga zimefumuana jioni hii katika makutano ya barabara ya Lumumba na Uhuru rodi (mnazi mmoja),ajali hiyo ilisababishwa na hilo daladala aina ya Isuzu Journey lenye nambari za usajiri T 670 ARQ ambalo lilikatiza katika makutano hayo likiwa na spidi ya ajabu na ndipo lilipokutana na hilo lori aina ya Isuzu Foward lenye nambari za usajiri T 217 ANR.baada ya kufumuliwa hiyo daladala nayo ilienda kuigonga daladala nyingine aina ya Toyota DCM lenye nambari za usajiri T 151 ABV na kusababisha uharibifu wa gari zote tatu.sasa sijui huyo mwenye hiyo Isuzu Journey alikuwa anawaza nini wakati anakatiza hapo??
Kuzuia ayo yote,ao dereva wa daladala waende shule.Na wenye magari Bongo wajaribu kuajiri watu wenye leseni halali.Now days in Dar kila mtu ni dereva,ukimuuliza wapi kasomea hakuna jibu.Magari ni vyombo vya moto sio vitu vya kuchezea.
ReplyDeleteMdau Finland