Napenda kutumia nafasi hii kuwatakia heri na fanaka ya sikukuu ya Eid El Fitr ndugu zangu waislamu na hata wasio waislam popote pale walipo katika Dunia hii kwa kuungana kwa pamoja kuisherehekea sikukuu hii,tunapaswa kumshukuru sana Mwenyezi mungu kwa kutujaalia kumaliza salama mfungo mtukufu wa Ramadhan kwa maana ni wengi walipenda kuwa pamoja nasi siku ya leo lakini kwa kurda za Mwenyezi Mungu Muumba mbingu na Ardhi hawakufanikiwa kufika leo.hivyo tunapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa hilo.tunapaswa kuisherehekea sikukuu hii kwa amani na utulivu mkubwa na tujitahidi tusifanye maasi katika siku hiyo maana kama itakuwa hivyo itakuwa umepoteza kabisa funga yako ya mwezi mzima.nawatakia kila la kheri katika hilo Inshaa - Allah
Eid Mubarak!
-Michuzi Jnr
No comments:
Post a Comment