

Globu ya Jamii inapenda kutoa shukran kareem kwa wote waliohudhuria futari hii ya kusherehekea hepi besdei ya anko nanihii katika hafla iliyofana sana.
Pia Globu ya Jamii inapenda kutoa asante za dhati kwa wadau wote waliotuma salamu za pongezi za siku hii ya kuzaliwa kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo FaceBook.
Ni vigumu kutoa asante kwa mdau mmoja mmoja kwa vile ni wengi mno, hivyo anko nanihii anaomba shukrani hizi ziwe kama wakala wa shukrani zake za dhati kwa wooooote waliotoa salamu za pongezi. Anawapenda sana.
Shukrani za pekee ziwaendee Tanzania Mitindo House walioandaa hafla hii ya futari na kula keki na pia Jose Mara wa FM Academia na mai waifu wake kwa kuandaa keki maalumu hiyo hapo juu.
Asanteni sana Jose, Monica na Hadija Mwanamboka pamoja na Asia Idarous kwa ukarimu wenu.Anko nanihii pia anatoa shukrani kwa bintiye Mamou pamoja na dada yake Zahra na kaka yao Maggid kwa kuungana naye kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na ndugu, jamaa na marafiki bila kuwasahau Juma Pinto na Ben Kisaka wa Jambo Leo, Kim Tenga, Da'Kabula wa TBL, Mariam Mogella na wenzie wa TSN, Saidi Tuli, Da'Mboni, na Dada Mishi wa Virago Boutique ya Namanga
pamoja wote na waliohudhuria.
-Michuzi
No comments:
Post a Comment