
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na mkurungenzi wa mawasiliano wa baraza la Maaskofu (TEC) kanisa katoliki, Padri Revocatus Makonge, Askofu huyo amefariki baada ya madaktari wa Hospitali ya rufaa ya Bugando kuhangaika kumpatia matibabu bila ya mafanikio.
Alisema kuwa marehemu aliamka salama jana na kuendelea na shughuli zake za kila siku ofisini kwake mpaka majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hospitali ya rufaa ya Bugando.
Habari kutoka katika ofisi ya askofu huyo, zimeeleza kuwa askofu huyo alipatwa na maradhi hayo wakati akiwa katika maandalizi ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Vatican ambaye alikuwa akitarajiwa kufanya ziara jimboni kwake Oktoba 5 mwaka huu kwa ajili ya kufungua ujenzi wa hospitali ya watoto.“Baada ya kufikishwa hospitalini hapo madaktari waliahangaika kuokoa maisha yake lakini bahati mbaya alifariki dunia majira ya saa 8:30 mchana,” alieleza Padri Revocatus Makonge.
Askofu Mayalla alizaliwa Aprili 23 mwaka 1940 katika kijiji cha Nera wilayani Kwimba na kupata elimu yake ya msingi katika wilaya hiyo na masomo ya sekondari.Askofu Mayalla alikuwa amehitimu shahada ya kwanza ya elimu aliyopata katika chuo kikuu cha Loyola huko Chicago Marekani mwaka 1973 hadi 1975.
Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Askofu Anthony Petro Mayalla.
Frederick Katulanda,
Mwanza.
No comments:
Post a Comment