HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 7, 2009

Msaada Unatakiwa Ili Kumnusuru Mtu Huyu

Mimi nina rafiki yangu yangu aitwaye MIM anampenda mtu lakini huyo mtu hampendi tena. Nasema hampendi tena kwa kuwa, hapo mwanzo alimpenda hasa na kumpa kila raha ya dunia( ndivyo asemavyo MIM) lakini, kutokana na uwongo mdogo alioutenda MIM, nao ni kumdanganya mpenziwe kuwa yu mgonjwa taabani ili mpenziwe ampe attention zaidi, huyo mpenzi wake aitwaye "S" amemkimbia na hamtaki tena.

MIM haelewi na kila njia alojaribu ili kurejesha penzi lake kwa S imeshindikana.

Nasema kila njia, kwani kamaliza waganga wote wa kitabu na tunguri, washauri na hata kamtumia watu wakamuombee msamaha kwa S lakini haikusaidia. Kwa mtazamo wake MIM hawezi kuishi bila S, na maisha hayana maana bila mpenzi wake huyo.

Niandikavyo hapa MIM amechanganyikiwa kimapenzi na tayari kajaribu kujiua mara mbili bila mafanikio, hivi sasa anaishi kwa kunywa dawa kali za matibabu ya kisaikolojia ili asichanyanyikiwe zaidi na kujaribu kujiua tena. Mimi ni rafiki mpenzi wa MIM na naomba ushauri wenu nimsaidie vipi rafiki yangu huyu.

Kwani hali yake ni mbaya, amerudi nyuma kimasoma na hata kushindwa kumalizia PHD yake. MIM ni msichana wa miaka 27 tu na S alikuwa mpenzi wake wa kwanza.Naomba ushauri wenu wadau ili nami niweze kumsaida rafiki yangu.

Natanguliza shukrani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad