HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 19, 2008

Teh Teh Teh!!!!!!!!!

Askari mmoja wa Marekani huko Afghanistan alipokea Barua toka kwa Girl friend wake, barua ilikuwa hivi:-

Mpenzi John samahani siwezi kuendelea na uhusiano wetu huu wa mapenzi kati yangu na wewe.Umbali uliopo kati yetu ni mkubwa sana pia nakiri kwamba nimekuwa sio mwaminifu kwako kwa kutembea nje mara nyingi tangia ulipoondoka na kwakuwa hakuna mtu aliye perfect basi huu ndio mwisho wa mapenzi yetu.Tafadhali nirudishie picha yangu niliyokutumia
salaam Wendy.

John alisoneneka sana na alivunjika moyo! baada ya kufikiri kwa muda John alienda kwa marafiki zake(askari wenzake) akakusanya picha za girl friends wao na ex girl friends wao,picha za dada zao,picha za binamu zao wa kike na picha za shangazi zao! jumla alipata picha 57.
Akaziweka pamoja na barua ya majibu kwa wendy ikisema hivi:-
Mpendwa Wendy samahani ni siku nyingi zimepita sikujui tena hivyo naomba utafute picha yako kati ya hizo na zinazobaki unirudishie.
wako! John.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad