HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 24, 2026

Waziri Mbarawa Aridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu Mipya ya CATC

 

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza jambo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa  Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika eneo la Banana, jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (Mb), ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mipya ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinachojengwa eneo la Banana, jijini Dar es Salaam, na kueleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo.

Hadi Julai 19, 2026, mradi huo ulikuwa umefikia asilimia 23.9 ya utekelezaji baada ya miezi 11 tangu kuanza kwa ujenzi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Prof. Mbarawa alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri K. Bakari, pamoja na Menejimenti ya TCAA, ambapo alipatiwa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi na hatua mbalimbali zilizofikiwa.

Mradi huo wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 78 unalenga kujenga miundombinu ya kisasa ya mafunzo ya usafiri wa anga, kuongeza uwezo wa Tanzania kuzalisha wataalamu wa sekta hiyo na kuimarisha nafasi ya nchi kuwa kitovu cha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.

Mhe. Prof. Mbarawa ameipongeza TCAA kwa usimamizi wa mradi huo, huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia viwango vya ubora pamoja na thamani ya fedha.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutakuwa hatua muhimu katika kuimarisha uwezo wa Tanzania katika kutoa mafunzo ya wataalamu wa usafiri wa anga na kuchangia maendeleo ya sekta hiyo nchini na barani Afrika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dkt. Jabiri K. Bakari (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa(kushoto) kuhusu mradi mradi wa ujenzi wa  Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika eneo la Banana, jijini Dar es Salaam
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akitembelea na kukagua maendeleo ya  mradi wa  ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) unaendelea katika eneo la Banana, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya majengo yaliofikia kwenye mradi wa  ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) unaendelea katika eneo la Banana, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad