HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 25, 2026

WAKULIMA WA KIPANDE-NKOAVELE KUONGEZEWA MITA 1000 YA MIFEREJI YA UMWAGILIAJI

 

WAKULIMA zaidi ya 650 katika kijiji cha Kipande-Nkoavele, Halmashauri ya Meru katika Mkoa wa Arusha kunufaika na mita 1000 za mifereji ya umwagiliaji kwa gharama ya Shilingi Milioni 200 ili kuendeleza matumizi ya kilimo cha umwagiliaji cha mazao ya mboga mboga na matunda.

Amesema hayo Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) tarehe 24 Julai 2026 na kuielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kukaa na timu yake ya Mkoa ili kuanza kazi ya kuongeza mfereji huo.

Mita hizo 1000 zinaenda kuongezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwenye ujenzi wa awali wa mifereji yenye urefu wa mita 612 iliyogharimu Shilingi Milioni 188.9 zilitolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kupitia mfuko wa OPEC II, III na IV. 

Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri Chongolo ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kujenga soko la kisasa ndani ya miezi saba (7) lenye sehemu ya uhifadhi wa baridi ili mazao ya mboga mboga na matunda yanayovunwa yaweze kuhifadhiwa kuepusha kuharibika kwa haraka.  

Sambamba na hilo, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imetoa ahadi kwa wakulima wa Halmashauri ya Meru kuwa itapeleka mbolea mapema hivi karibuni ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji wa mazao kwa ubora zaidi.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad