HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 25, 2026

CHONGOLO: ARUMERU NAJUA MNACHOKITAKA NI MAENDELEO

 




WANANCHI wa Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha wamepewa shimishimi ya kuendelea na shughuli za kiuchumi kwa kuwa ahadi za Serikali kuwaletea maendeleo zitatekelezwa.

Amesema Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Arusha tarehe 24 Julai 2026 ambapo amekagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ni barabara wa KIA-Usa River; ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya kijiji cha Kipande-Nkoavele; uzinduzi wa mabweni, madarasa na vyoo katika Shule ya Sekondari ya Mlangarini na mkutano wa hadhara wa eneo la Usa River.

Amepongeza wananchi hao ambao asilimia 90 ni wakulima wa kilimo cha umwagiliaji cha mazao ya mboga mboga na matunda (horticulture) katika Halmashauri ya Meru.

“Nimewasikia kilio chenu cha kuongezewa mita 1000 za mifereji ya umwagiliaji hivyo nimeielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kutoa Shilingi Milioni 200 kugharamia ujenzi huo,” amesema Waziri Chongolo.

Kuhusu ombi la kujengewa soko na chumba cha ubaridi cha kuhifadhi mazao, Waziri Chongolo ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kufanya taratibu za ujenzi wa soko hilo ndani ya miezi saba (7).

Wakati wa ziara yake, Waziri Chongolo amekagua pia barabara wa KIA-Usa River; ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya kijiji cha Kipande-Nkoavele; uzinduzi wa mabweni, madarasa na vyoo katika Shule ya Sekondari ya Mlangarini na kufanya mkutano wa hadhara na mamia ya wananchi waliojikusanya katika eneo la Usa River.

Viongozi mbalimbali walioshiriki katika ziara hiyo ni pamoja Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Dkt. Toba Alnason Nguvila; Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi; Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mhe. Joshua Nassari; Mbunge wa Arumeru Magharibi, Mhe. Dkt. Johannes Lembulung Lukumay; Wakurugenzi wa Wizara ya Kilimo na Taasisi zake.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad