
Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi Maonesho ya 50 ya Biashara Kimataifa Rais wa Msumbiji Daniel Francisco Chapo akimkabidhi Mwakilishi wa Kampuni ya GF Truck Salman Karmal Tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa Banda Bora katika Maonesho ya 50 ya Biashara Kimataifa ,jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya GF Trucks imesema katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) imepata mafanikio ya kuaminika kwa ubora baada ya kutwaa tuzo ya banda bora kwa mwaka wa pili katika maonesho hayo
Mafanikio hayo yanaelezwa kutokana na kuendelea kuendelea katiika kuleta teknolojia bunifu na rafiki kwa mazingira nchini.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mwakilishi wa kampuni hiyo, Salman Karmali, amesema mafanikio hayo ni ishara ya imani ambayo kampuni imejijengea kwa wadau na wananchi kupitia ushiriki wake wa muda mrefu katika maonesho hayo.
Amesema GF Trucks and Equipment imekuwa mshiriki wa maonesho ya Sabasaba kwa miaka mingi na imeendelea kutumia jukwaa hilo kuwatambulisha Watanzania bidhaa na teknolojia mpya zinazolenga kuongeza ufanisi katika sekta Usafirishaji pamoja na mitambo.
Mwaka huu wa maadhimisho ya miaka 50 ya Sabasaba, GF Trucks and Equipment imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuleta suluhisho za kisasa katika sekta ya usafirishaji, ujenzi na uchimbaji, huku ikijikita katika matumizi ya teknolojia endelevu na rafiki kwa mazingira.
“Ni heshima kubwa kwetu kupata tuzo hii kwa mwaka wa pili mfululizo. Tunawashukuru viongozi wa TanTrade kwa kutupa heshima hii na kutuongezea hamasa ya kuendelea kuboresha huduma na bidhaa zetu,” amesema.
Amebainisha kuwa katika maonesho ya mwaka huu kampuni imewasilisha bidhaa mbalimbali zikiwemo magari madogo, malori, mitambo mizito pamoja na mashine za kisasa za utafiti na uchimbaji maji.
Amesema vivutio vikubwa katika banda lao ni mitambo pamoja na mashine za utafiti na uchimbaji zinazojulikana kama drilling rigs au exploration rigs, ambazo hutumika katika tafiti za vyanzo vya maji na shughuli nyingine za uchimbaji.
Amesema baadhi ya mitambo hiyo imebuniwa kwa kuzingatia mazingira na mahitaji ya Tanzania baada ya kufanyiwa tafiti za kina ili kuhakikisha inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Karmali amesema kampuni hiyo inaendelea kuunga mkono juhudi za kuhifadhi mazingira kwa kuleta teknolojia zinazopunguza matumizi ya mafuta na kupunguza athari kwa mazingira.
“Kwa sasa dunia inaelekea kwenye matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira. Sisi tumekuja na bidhaa zenye matumizi madogo ya mafuta na pia tumewaletea magari yanayotumia umeme ya chapa ya Hyundai, ambayo tayari yameanza kutambulishwa nchini,”amesema.
Ameongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa ofa maalum kwa wateja wake hadi mwisho wa maonesho hayo na kuwahimiza wananchi pamoja na wadau wa sekta mbalimbali kutembelea banda lao ili kujionea teknolojia mpya zinazowasilishwa na kampuni hiyo.
Mwakilishi wa Kampuni GF Truck & Equipment akiwa katika ufunguzi wa maonesho ya 50 ya Biashara Kimataifa


No comments:
Post a Comment