SERIKALI imeagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha inasimamja usambazaji wa mbolea kwa wakulima nchini wakiwemo wakulima wa kijiji cha Mang’ola, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Amesema Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo tarehe 22 Julai 2026 ili kukagua miradi ya maendeleo.
“Niwapomgeze wananchi wa Mang’oa kwa kujishughulisha na kilimo cha vitunguu na mazao memgime. Nimeielekeza TFRA na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuhakikisha mbolea inayosambazwa nchini inawafikia,” amesema Waziri Chongolo.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Bw. Samwel Mshote amesema kuwa tani elfu mbili za mbolea ya DAP zinapelekwa ndani ya wiki mbili katika kijiji hicho huku taratibu za kuwa na myrndaji wa TFC kuwepo Mang’oa zitatekelezwa ili wakulima wapatiwe elimu ya matumizi sahihi ya mbolea.
Sambamba na hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Joel Lauren amesema kuwa wakulima wataendelea kupatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea kupitia Kampeni ya Mali Shambani inayoratibiwa na Wizara ya Kilimo kuanzia mwezi Agosti 2026 .
Ameeleza kuwa “matumizi mbadala si kununua mbolea kwa jina badala yake ni kuwa na elimu ya sahihi ya matumizi ya mbolea kwa kuendana na virutubisho, afya ya udongo na mbegu bora.”
Kuhusu biashara holela ya mbolea, Bw. Laurent amesema kuwa hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza mbolea kinyume na masharti ya leseni yake na moja ya adhabu ni kufutiwa leseni. Mpango wa ruzuku bado upo kupitia maelekezo ya Serikali ambayo imetoa fedha kuhakikisha mkulima anapata bei himilivu ya mbolea.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

No comments:
Post a Comment