HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 2, 2026

Serengeti Apple Yawakutanisha Wadau kwa Mkakati Maalum Kuelekea Uzinduzi Unaosubiriwa kwa Hamu

Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imewakutanisha wadau kutoka tasnia mbalimbali kama vile ulimbwende, mavazi, ubunifu, ujasiriamali na taaluma tofauti katika mkakati maalum, ambapo walipata fursa ya kufahamishwa kwa undani kuhusu kinywaji kipya cha Serengeti Premium Apple, kinachozalishwa hapa nchini Tanzania.

Kikao hicho kilichofanyika katika mgahawa maridadi wenye hadhi ya kipekee wa Upper Deck jijini Dar es Salaam, ni sehemu ya utaratibu wa kampuni ya SBL wa kuandaa na kuratibu uzinduzi wa bidhaa zake, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha wadau muhimu wanaelewa na kuendana na mwelekeo wa chapa husika kabla ya matukio makubwa na shughuli tofauti zitakazoambatana nazo. 

Washiriki walipatiwa maelezo ya kina kuhusu historia ya chapa, nafasi yake sokoni, pamoja na maono ya Serengeti Premium Apple na kile inachowakilisha kwa walaji wa kisasa wa Kitanzania wanaotafuta uzoefu wa kijamii wenye hadhi ya juu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Bw. Wema Mugofwa kutoka SBL, alieleza umuhimu wa bidhaa hiyo mpya pamoja na nafasi ya wageni na wadau waalikwa kuelekea safari ya uzinduzi wake hivi karibu mahali ambapo panatajwa kuwa pa kipekee na haijawahi kufanywa na chapa yoyote nchini:

“Serengeti Premium Apple ni ishara mpya ya dhamira yetu ya kuendeleza ubunifu na ubora wa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini. Kama kinywaji chenye ladha ya kipekee na hadhi ya juu kilichotengenezwa Tanzania, kinaakisi mabadiliko ya ladha na mahitaji ya wateja wa kisasa, wanaothamini ubora, mtindo wa maisha, na uhalisia wa mazingira wanayoishi. 

Tunapojiandaa kwa uzinduzi rasmi, tunafurahia kushirikiana na wabunifu wa maudhui ambao watasaidia kusimulia hadithi hii kwa njia halisi, inayovutia na yenye kuendana na hadhira yao na Watanzania wengi kwa ujumla,” alisema Bw. Mugofwa.

Mbali na kupata elimu na ufahamu kuhusu chapa hiyo, kikao hicho pia kilitoa nafasi ya majadiliano ya wazi, ambapo wadau na wageni waalikwa waliweza kuzungumza moja kwa moja na timu ya masoko ya kampuni ya SBL, kuuliza maswali, na kupata ufahamu wa kina kuhusu mwelekeo wa uzinduzi pamoja na shughuli ambazo zinatarajiwa kufanyika.

Wengi wa wageni waalika walionesha shauku na matarajio makubwa ya kuwa sehemu ya uzinduzi huo, huku wakivutiwa na shughuli na matukio yaliyoandaliwa kwa ubunifu wa kipekee wakati wa kikao hicho.

Kwa sasa, maandalizi yakiwa yamekamilika na kasi ya hamu ya kujua kitakachofanyika ikiongezeka, mazingira yameandaliwa vema kwa tukio ambalo tayari limeanza kuvutia hisia za wengi, na ambalo wengi wanatamani kushiriki na kulishuhudia moja kwa moja, kwasababu historia inaenda kuandikwa upya. #serengetiapple #ProudlyTanzanian @serengeti.apple











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad